Kocha wa klabu ya Simba Roberto Oliviera maarufu kama Robertinho ambaye alienda kwao Brazil siku kadhaa nyuma sasa amerejea rasmi nchini Tanzania kuendelea na majukumu yake klabuni hapo.
Klabu ya Simba ilitangaza kua kocha wake Robertinho kuondoka nchinina kuelekea nchini Brazil ambapo walieleza kua kocha huyo atarejea nchini mwishoni mwa mwezi Januari, Leo mapema mchana kocha huyo ameonekana akirejea nchini Tanzania.
Klabu ya Simba ilikua chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda huku kocha huyo akiwa kwao nchini Brazil, Taarifa zinaeleza kocha huyo alielekea nchini Brazil kwajili ya kumalizia pragramu maalumu ya yeye kupata leseni kubwa ya ukocha maarufu kama Pro License.
Kocha Robertinho sasa amerejea rasmi katika klabu ya Simba na ataanza na maandalizi ya kukiandaa kikosi hicho kwajili ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo inatarajiwa kuanza ndani ya mwezi unafuata yaani mwezi wa pili.
Kocha Robertinho ikumbukwe alikuja ndani ya klabu ya Simba kwa lengo kubw ala kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Na kocha huyo aliahidi kua klabu hiyo inaweza kufika hatua ya nusu fainali hata ikiwezekana hatua ya fainali.

