Klabu ya Man United imefanikiwa kuzindua jezi zake za nyumbani kwa kuwatumia nyota wao kadhaa katika uzi utakaotumiwa katika msimu wa 2021/2022.
Miongoni mwa wachezaji waliotumiwa katika kuonesha jezi hizo ni beki bora wa kushoto Luke Shaw, Marcus Rashford, Paul Pogba, Harry Maguire na Juan Mata.

Katika jezi hizo, ile logo iliyozoeleka ya Chevrolet imeondolewa na TeamViewer ambao walifanikiwa kununua zabuni ya jezi kwa mwaka huu na kuwapiku Chevrolet ambao wamekuwa wakifanya kazi na Man United kwa muda sasa!
Baada ya kuzindua jezi hiyo kurasa za Man United zilieleza kuwa kuchagua kwa jezi hizo kwa rangi na maandishi ni kuenzi mafanikio makubwa ya klabu hiyo na mji wa Manchester ulivyokuwa kwa pamoja.
Jezi hizo pia za Man United zimeelezwa kuwa zimetokana na kuenzi wachezaji wa zamani ambao walichezea aina hiyo hiyo ya jezi za nyumbani, na wachezaji nguli wa klabu hiyo kama George Best, Sir Bobby Charlton na Denis Law.

Manchester United wataanza kibarua cha ligi kuu ya Uingereza EPL agosti 14 dhidi ya Leeds United.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



dorophina
Uzi umetulia