Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Leeds United mchezo utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.
Manchester United itakua dimbani leo kuhakikisha kua wanaendeleza rekodi yao ya kushinda michezo katikia dimba lao la Old Trafford, Klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kushinda katika dimba la Old Trafford michezo 13 mfululizo mpaka sasa.Klabu ya Man United watawakaribisha Leeds United ambao wametoka kufukuza kocha wikiendi iliyomalizika na kuufanya kua mchezo mkali na wenye ushindani mkubwa. Man United wao watahitaji kuendelea kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Klabu ya Leeds wao ambao wametoka kupoteza mchezo wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Nottingham Forest mpaka kupelekea kufukuza kocha wao Jesse Marsch, Hivo mchezo huu utakua muhimu zaidi kwa klabu hiyo ili kuweza kujitoa kwenye hatari ya kushuka daraja.Klabu ya Manchester United ikifanikiwa kushinda mchezo wa leo dhidi ya Leeds United itaweza kulingana alama na mahasimu wao klabu ya Manchester City ambao wana alama 45 mpaka wakati huu, Hivo mashetani hao wekundu watahitaji alama tatu za leo kwa uchu mkubwa.