Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC upande wa wanachama, Murtaza Mangungu amesema mageti ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yatafunguliwa saa tisa alasiri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates Jumapili.

Mangungu amewaomba mashabiki waendelee kununua tiketi kwa wingi ili kuujaza uwanja kwakua tumepewa fursa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuujaza uwanja.

 


Wachezaji wa Simba SC Mazoezini.

“Mageti yatafunguliwa saa tisa alasiri siku ya mchezo kwa kuwa uwanja utakuwa na matumizi mengine ya usomaji wa Quran kwa hiyo usitoke nyumbani ukafikiri utaingia mapema,” amesema Mangungu.

Mwenyekiti Mangungu ameongeza kuwa wanaobeza jitihada zao katika kuingiza timu nne kwenye michuano ya Afrika kwa mara ya pili mfululizo wana nongwa.

“Kwa miaka miwili tunaingiza timu nne kwenye michuano ya Afrika lakini watu wanajifanya hawaoni hizo tunaita nongwa,” aliongeza.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa