Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 28, anatazamiwa kuachana na mpango wa kuhamia Manchester United msimu huu wa joto na kusalia Tottenham.

Tetesi zinasema, Meneja Mholanzi, Ten Hag ameweka wazi kwa uongozi wa Manchester United kwamba mshambuliaji nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, hatafaa mtindo wake wa uchezaji.

Beki wa kulia wa Norwich Max Aarons analengwa na United na Arsenal, wakati Bayern Munich na Borussia Dortmund pia wanamfuatilia Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 20.

 

Max Aarons

Tetesi zinasema Newcastle inamsajili beki wa kati wa Sevilla, Mbrazil Diego Carlos, 29 kamaa mbadala wa Sven Botman endapo ataelekea AC Milan.

Manchester City wamemfanya kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 22, kuwa mlengwa wao mkuu msimu huu kuchukua nafasi ya Fernandinho anayeondoka.

Borussia Dortmund wamefuzu katika harakati zao za kumsaka mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Mjerumani Karim Adeyemi, 20, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Liverpool.

Tottenham wana nia ya kumsajili Lautaro Martinez wa Inter Milan msimu huu wa joto baada ya kumkosa Januari, lakini wana kabiliwa na ushindani kutoka kwa Atletico Madrid kumnunua mshambuliaji huyo wa Argentina, 24.

 

Lautaro Kufikia Makubaliano Mapya na Inter.

Tetesi zinasema, Villarreal wapo tayari kwa mazungumzo na Tottenham kuhusu uhamisho wa kudumu wa Giovani lo Celso baada ya kuwa na kiungo huyo wa Argentina, 26, kwa mkopo tangu Januari.

Manchester City bado wanasubiri kupokea majibu ya ofa zao za kandarasi mpya kwa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 31, mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 27, na mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 25.

Brentford wamezungumza na Shakhtar Donetsk kuhusu usajili wa wachezaji wawili wa Ukraine, winga wa miaka 21- Mykhaylo Mudryk na mlinzi wa safu ya kushoto Mykola Matviyenko, 25, msimu huu wa joto.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa