Marc Overmars Ajiuzulu Ajax.

 

Mkurugenzi wa Soka wa klabu ya Ajax, Marc Overmars, mkurugenzi wa amejiuzulu katika nafasi hiyo baada ya kutuhumiwa kutuma msururu wa jumbe zisizofaa kwa wenzake kadhaa wa kike.

 

Ajax wamesema kuwa Overmars alichukua uamuzi wa kujiuzulu baada ya mazungumzo ya siku za hivi karibuni na bodi ya klabu na mtendaji mkuu Edwin van der Sar.

Overmars ambaye ni winga wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Ajax – aliiambia tovuti ya klabu: “Nahisi aibu. Wiki iliyopita nilikabiliwa na ripoti kuhusu tabia yangu na jinsi hii imetokea kwa wengine.

“Kwa bahati mbaya, sikugundua kuwa nilikuwa navuka mipaka kwa hili, lakini hilo liliwekwa wazi kwangu katika siku za hivi karibuni. Ghafla nilihisi shinikizo kubwa. Ninaomba msamaha.

“Hakika kwa mtu katika nafasi yangu, tabia hii haikubaliki. Sasa naona hivyo pia. Lakini nimechelewa. Sioni njia nyingine zaidi ya kuondoka Ajax.

“Hii pia ina athari kubwa kwa hali yangu ya faragha. Ndiyo maana ninaomba kila mtu aniache peke yangu na familia yangu.” aliongeza.

Overmars alikuwa ameshikilia nafasi ya mkurugenzi wa masuala ya soka kwa takriban miaka 10, hivi karibuni kandarasi yake iliongezwa hadi mwisho wa msimu wa 2025/26.


EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe