Mchezaji wa klabu ya Arsenal raia wa Brazil Gabriel Martinelli amekaribia kusaini mkataba mpya ndani ya klabu ya Arsenal wakati huu mazungumzo yakiwa yanaenda vizuri kwa pande zote.
Mshambuliaji huyo ambaye ametoka kuiwakilisha timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia iliomalizika hivi karibuni, Klabu ya Arsenal inahitaji kumuongezea mkataba mpya ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.
Mazungumzo kati ya upande wa Martinelli na klabu ya Arsenal yanaenda vizuri na inataarifiwa yako kwenye hatua za mwisho kabisa na mchezaji huyo ataongeza mkataba wa kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo baada ya kila kitu kukamilika.
Mshambuliaji huyo amabye ameonekana kufanya vizuri zaidi chini ya kocha Mikel Arteta, Na inaelezwa kocha huyo ndio amependekeza kuongezewa mkataba kwa mchezaji huyo kwakua ana mipango nae ya muda mrefu klabuni hapo.
Klabu ya Arsenal imepenga kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu klabuni hapo ukiachana na Gabriel Martinelli, Klabu hiyo pia inataka kuwaongezea mikataba wachezaji kadhaa akiwamo Bukayo Saka, na William Saliba.

