Conte Kutowapa Mapumziko Marefu Mastaa waliotoka Kombe la Dunia

Kocha wa Klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amesema sio rahisi kuwapumzisha mastaa wake 12 waliotoka kwenye michuano ya kombe la dunia hivi karibuni.

Kikosi cha Tottenha kitamenyana na klabu ya Brentford siku ya jumanne huku ikiwa ni siku nane tu baada ya wachezaji wake wawili kucheza mchezo wa fainali ya kombe la dunia ambao ni nahodha Hugo Lloris na beki Christian Romero, Lloris anatarajiwa kua kwenye benchi siku ya jumanne huku Romero hatakuepo kwenye kikosi.conteKocha wa klabu hiyo Antonio Conte amesema kua itakua ngumu kwa yeye kuwapa muda mrefu wa kupumzika mastaa wake waliotoka kwenye michuano hiyo, Kwasababu ya watakosa utimamu wa mwili kulingana na michezo ambayo inawakabili hapo mbeleni.

Lakini kocha huyo amefurahishwa na namna klabu yake ilivyofanikiwa kutoka wachezaji 12 kwenye michuano ya kombe la dunia, Akieleza kulingana na idadi hiyo inaonesha wako kwenye njia sahihi ambayo inaonesha wako kiushindani na wanaweza kushinda kitu.conteKocha Antonio Conte amesema wachezaji aliokua nao kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hawakushiriki michuano ya kombe la dunia wana utimamu wa kimwili tofauti wale walioshiriki, Hivo jambo hilo linamfanya asiwape mda mrefu wa kupumzika wachezaji wake hao ili waweze kurudisha utimamu wa mwili mapema.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.