Klabu ya Simba SC leo itashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuikabili ASEC Mimosas katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

simba, Match Day : Simba SC vs ASEC Mimosas., Meridianbet

Malengo ya Simba SC katika hatua ya makundi ni kuhakikisha wanapata alama tatu katika mechi zote za nyumbani na kutafuta sare moja ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali.

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco amesema mchezo utakuwa mgumu na mzuri kutokana ubora wa wapinzani wao lakini maandalizi waliyofanya ukilinganisha na kutumia uwanja wa nyumbani anaamini wataibuka na ushindi.

“ASEC ni timu bora na ina uzoefu mkubwa katika michuano hii ya Afrika lakini tupo tayari kuhakikisha tunafanya vizuri katika uwanja wetu wa nyumbani,” amesema Pablo.

Agosti 24 mwaka 2003 Simba SC ilikutana na ASEC katika mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa ambapo mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa bao moja.

Mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Ivory Coast walipoteza kwa mabao 4-3 na kukosa nafasi ya kuingia nusu fainali.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa