Staa wa Ufaransa na Klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameongelea taarifa ya watu wengi inayosema yeye ni raia wa Kameruni badala ya Ufaransa.
“Mimi siyo mKameruni #🇸🇳. Mimi ni mFaransa #🇫🇷. Mwanzoni kabisa wakati nimeanza kujihusisha na soka, wakati bado kiza kimetanda mbele yangu, baba yangu aliwasiliana na ‘Fecafoot’ ili waweze kunipa nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya Kameruni.

Wakamtaka atoe kiasi kikubwa cha pesa ili mimi niweze kuchezea timu hiyo. Baba yangu ambaye hakupendezwa na kitendo hicho akaamua kuhamishia majeshi Ufaransa, Ufaransa hii ambayo imenipa nafasi ya kuuonesha ulimwengu uwezo nilionao katika soka.
Leo sasa nimekuwa mchezaji mwenye gharama zaidi Duniani ndipo Kameruni wananipigia simu na kunipa utaifa ambao sio wangu. Mimi ni mFaransa na nitabakia kuwa mFaransa.” amesema Mbappe
Ikumbukwe Kylian amezaliwa Bondy, kaskazini-mashariki mwa jiji la Paris, Ufaransa. Wazazi wake Mzee Mkameruni Wilfried Mbappe (ambaye alikuwa kocha) na Mama yake MuAlgeria, Fayza Mbappe.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



Shakila mrope
Ooh kumbe vizuri
Issa
Si mzalendo
Saupha mohamed
Mbappe mtu mbaya
Adelta
Mbappe Yuko makini Sana
Sarah
Tumekuelewa mbappe
Hopemwaikuka
Wakamerun achen shobo
Tatu
Mbona hvyo
Lydia Emmanuel Magoti
Mbappe yupo sahii
Mwanahamisi
Mbappe yuko juu
Fatuma kasomo
Gud news
Caroline
Asante kwa kutujulisha
Theonestina
Ni kweli
Rahmal
Sawa mbappe tumekuelewa
warda
Bora alivyowakatalia wao mwanzo si walimkataa
Chiku
Dawa ya moto ni moto