Milan Yampeleka Bennacer kwenda Olympique Marseille Wakiwa na Chaguo la Kumnunua

Milan imemkabidhi rasmi kiungo Ismael Bennacer kwa Olympique Marseille kwa mkopo na chaguo la kumnunua mwishoni mwa msimu huu.

Milan Yampeleka Bennacer kwenda Olympique Marseille Wakiwa na Chaguo la Kumnunua

Kulingana na ripoti mbalimbali, makubaliano hayo ni ya ada ya mkopo ya €1m, basi kuna chaguo kuyafanya kuwa ya kudumu mnamo Julai 2025 kwa €12m zaidi pamoja na €3m ya bonasi.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Milan kutoka Empoli msimu wa joto wa 2019 kwa gharama ya €17.2m na akaendelea kucheza mechi 178 za ushindani kwa kilabu, akifunga mabao nane na kuchangia 12.

Milan Yampeleka Bennacer kwenda Olympique Marseille Wakiwa na Chaguo la Kumnunua

Bennacer alizaliwa na kukulia nchini Ufaransa, hivyo hii ni kurejea kwa mchezaji huyo ambaye aliondoka kwenda katika akademi ya vijana ya Arsenal mwaka 2015 na amekuwa Italia tangu 2017 huko Empoli na kisha Milan.

Amebadilishwa katika kikosi cha Rossoneri na Warren Bondo, ambaye alikamilisha uhamisho wa kudumu kutoka Monza leo kwa Euro milioni 10 pamoja na nyongeza, huku Kevin Zeroli pia akijiunga na Monza kwa mkopo.

Acha ujumbe