Niyonzima Afunguka Kuikosa Kariakoo Dabi.

 

Kiungo fundi wa mpira wa Yanga, Haruna Niyonzima amevunja ukimya baada ya sintofahamu iliyojitokeza kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba.

 

Niyonzima amesema anashindwa kuelewa utovu wa nidhamu aliouonyesha kwani alikuwa anaumwa na kusababisha kukosekana katika safari ya mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Biashara United mkoani Tabora.

“Nilikuwa ninaumwa na dozi yangu ya dawa ilimalizika juzi Jumatatu, siku iliyofuata nilikuwa niingie kambini, lakini wakati najiandaa kwenda nilipata ujumbe kwamba sitakiwi kwenda na sasa sitakuwepo kwenye mipango ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba.

 

“Baada ya taarifa hiyo nilihoji sababu ni zipi, lakini sikupata jibu hivyo nikaona busara ni kukaa kimya.”amesema Niyonzima.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe