Klabu ya Tottenham wamemteua bosi wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo kama meneja wao mpya kwa kandarasi ya miaka miwili.
Nuno aliondoka Wolves mnamo Mei baada ya misimu minne kufanya vizuri, wakati huo alipochukua klabu na kuipeleka Robo fainali ya Ligi ya Europa.
Spurs ilimtimua Jose Mourinho mnamo Aprili na nafasi yake kuchukuliwa na Ryan Mason mwenye umri wa miaka 29 hadi mwisho wa msimu uliopita.
“Ni raha kubwa na heshima [kuwa Spurs]. Nina furaha na ninatarajia kuanza kazi,” alisema Nuno.
“Hatuna siku za kupoteza na lazima tuanze kufanya kazi mara moja kabla ya msimu kuanza katika siku chache.”
Nuno hatasubiri sana kukutana na klabu yake cha zamani kwani Spurs wana safari ya kwenda Molineux kumenyana na Wolves kwenye mchezo wao wa pili wa ligi msimu huu tarehe 22 Agosti.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

