Orodha ya Wachezaji Huru Inavutia!

Julai 1, 2021 inaweza kuwa ni tarehe ya faida na pengine ni maumivu kwa baadhi ya vilabu. Orodha ya wachezaji huru inavutia!

Baadhi ya wachezaji wamemaliza mikataba yao usiku wa kuamkia Julai 1 na sasa ni rasmi, wachezaji hao wapo huru kujiunga na klabu yeyote ulimwenguni.

Lionel Messi anaongoza orodha ya wachezaji huru ikiwa ni dhahiri, baada ya sakata lake la kutaka kuondoka Barcelona kubuma mwaka jana, ameutumikia muda wa mwaka 1 uliokuwa umebaki kwenye mkataba wake na klabu hiyo. Kutokana na kwamba bado Messi hajaongeza mkataba mpya na Barca, ni rasmi sasa anaweza kuamua kubaki Camp Nou au kwenda klabu nyingine yeyote. Mazungumzo ya mkataba mpya yanaendelea na pengine lolote linaweza kutokea.

Sergio Ramos, beki huyu ameitumikia Real Madrid kwa miaka 16 lakini kwa sasa ni rasmi yupo huru kujiunga na klabu yeyote baada ya mkataba wake na Madrid kukoma. Ramos alishaagwa na uongozi wa Madrid na kwa sasa yupo nje ya uwanja akisubiri timu inayomuhitaji.

Juan Mata, japokuwa hajapata muda mwingi wa kuonesha uwezo wake uwanjani akiwa na Ole Gunnar Solskjaer msimu uliopita. Mata anaongezeka kwenye orodha ya wachezaji huru barani ulaya. Mazungumzo ya mkataba mpya yanaendelea na pengine lolote linaweza kutokea.

Lee Grant, mkataba wa golikipa huyu wa Man United umehitimishwa jana usiku lakini, kuna sintofahamu kuhusu hatma ya David De Gea na Dean Henderson. United watamtangaza Tom Heaton kama golikipa mpya muda wowote kuanzia leo na hivyo uwezekano wa Grant kusalia United utategemea hatma ya De Gea na Henderson, endapo mmoja ataondoka basi ni dhahiri Grant anaweza akafikiriwa upya.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.