Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco ameweka wazi kuwa pointi tatu walizopata katika mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting ni muhimu na zitaongeza hali ya kujiamini kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Pablo amesema timu ilicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na kupata mabao matatu ambapo pia tulitengeza nafasi nyingi ambazo zingetufanya kupata ushindi mnono zaidi.
Katika mchezo huo Medie Kagere alifunga bao la kwanza dakika ya 17 baada kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Bernard Morrison. Kabla ya kuongeza tena bao la pili dakika ya 36 baada ya kumalizia mpira uliookolewa na mlinda mlango Mohamed Makaka kufuatia shuti kali la mguu wa kushoto na Kibu Denis.
Kibu alifunga bao la tatu dakika ya 44 akimalizia mpira wa kisigino uliopigwa na Kagere baada ya shambulizi zuri tulilofanya langoni mwa Ruvu. Wakati Elius Maguli aliipatia Ruvu bao lao dakika ya 70 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shaban Msala kufuatia walinzi wetu kuzembea kuondoa hatari.
Pablo ameongeza kuwa Simba SC ni timu kubwa na inastahili kupata zaidi ya tulichokipata leo hivyo tutaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kuwa imara.
“Ni ushindi muhimu tumepata, nilizungumza na wachezaji kuhusu hili, tunajua utaongeza morali kuelekea mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows.
“Tulicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini tunastahili kupata zaidi, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kurudi kwenye ubora wetu hivyo tunapaswa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza,” amesema Kocha Pablo.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.