Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco, amesisitiza kuwa katika mchezo wa kesho dhidi ya Red Arrows tunapaswa kuwa makini kutumia nafasi tutakazopata na kuimarisha ulinzi na kupunguza makosa.

Pablo amesema mchezo bado haujamalizika licha ya kuwa wana mtaji wa mabao matatu tuliyopata kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam siku chache zilizopita.
Kocha huyo anaamini Red Arrows wataingia kwa kushambulia kwa kuwa hawana wanachohitaji zaidi ya mabao ili kufuzu hatua ya makundi hivyo amesisitiza umakini muda wote.
“Tunahitaji kuwa makini muda wote. Nafasi tukazopata tunatakiwa kuzitumia, wapinzani wataingia kwa nguvu kuhakikisha wanapata mabao, wao hawana cha kupoteza na watakuwa na faida ya kucheza nyumbani hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari.
“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji bora, tumejipanga vilivyo kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kuingia hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika,” aliongeza Pablo.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


