Klabu ya RB Leipzig wamekubaliana na kocha wake mkuu Jesse Marsch kuvunja mkataba baada ya kupoteza kwa 2-1 dhidi ya Union Berlin siku ya ijumaa kwenye mchezo wa ligi kuu ua Ujerumani Bundesliga.
Kocha wa msaidizi Achim Beierlorzer atachukua majukumu yalioachwa na Jesse na ataiongoza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City siku ya Jumanne.

“Haikuwa laisi kuachana na Jesse, sababu nilikuwa namchukulia Jesse kama mtu muhimu, ni aibu kwa kuwa mambo hayakwenda sawa, kama tulivyokuwa tunatumaini, hatua zaidi zilihitajika, kwa bahati mbaya maendeleo tuliyo yatarajia na matokeo ya mafanikio hayakufikiwa.” Oliver Mintzlaf mkurugenzi mkuu wa Leipzig.
Marsch alijiunga na RB Leipzig msimu huu akichukua nafasi ya Julian Nagelsmann ambaye alijiunga na klabu ya Bayern Munich, Jesse alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Leipzig, pia aliwai kufanya kazi kama msaidizi wa Ralf Rangnick mwaka 2018/19 akiwa kocha mkuu Leipzig, kabla kwenda kuchukua mikoba ya kuiongoza Red Bull Salzburg.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


