Paul Scholes: Sikua Bora kama Mainoo

Kiungo gwiji wa zamanin wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Paul Scholes amemsifia kiungo kinda wa klabu hiyo Kobbie Mainoo kua yeye hakua bora kama kinda huyo.

Baada ya mchezo wa fainali ya Fa Cup jana kumalizika na Manchester United kutwaa taji hilo na Mainoo kua moja ya wafungaji ndipo Paul Scholes aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kua Mainoo amekua bora kuliko yeye kwenye umri wa miaka 19.paul scholes“Nilisoma ulinganisho baina yangu na kijana Mainoo wiki kadhaa zilizopita msipoteze muda wenu yeye ni bora mara ya kumi ya nilivyokua kwenye umri wa miaka 19,Napenda anavyopokea mpira, utulivu wake, Lakini pia kutambua kina wanamzunguka, pia kufunga magoli katika michezo mikubwa huyu kijana ni wa kipekee” Alisema Paul Scholes.

Kijana Kobbie Mainoo amekua na msimu bora sana ndani ya kikosi cha Manchester United licha ya umri wake kua mdogo wa miaka 19 tu, Lakini tayari ameshaonesha ana kila sababu ya kua mchezaji mkubwa siku za usoni kwani hata wakongwe na wachezaji wenzake wameongea mara kadhaa ubora wake.paul scholesMsimu huu umekua wa mafanikio kwa kijana huyo kwani ndio msimu ambao amepata nafasi kuanza mchezo wake wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini pia kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza na kuanza pia kwenye timu hiyo haya yote yanathibitisha maneno ya gwiji Paul.

Acha ujumbe