Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag baada ya kufanikiwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji la Fa mbele ya mahasimu wao Man City lakini pia aliwatolea uvivu waandishi wa habari.
Kocha Ten Hag ameonesha kuchukizwa na tabia ya waandishi wa habari nchini Uingereza kua wepesi kusifia, Lakini pia kua wepesi kuwaponda makocha na wachezaji pale ambapo yanakua hayaendi sawa kidogo.Baada ya mchezo wa fainali kocha huyo alifanya mazungumzo na kituo kimoja kikubwa nchini humo na kuulizwa juu ya muenendo wa timu yake ulivyokua ndani ya msimu huu.
Kocha huyo aliweka wazi msimu huu ameandamwa na majeraha kwenye kikosi chake kwa kiwango kikubwa na wachezaji wake muhimu wengi walikua nje jambo ambalo lilifanya wao kufanya vibaya, Lakini wanahabari hawaongelei zaidi wanajikita kwenye kukosoa.Kocha Ten Hag alisisitiza kama anakua na wachezaji wake muhimu mara nyingi amekua akipata matokeo chanya kama ambavyo jana amefanikiwa kutwaa taji la Fa, Hivo amewataka waandishi kupunguza kukosoa zaidi pale mambo yanapokua hayaendi sawa.