Amrabat Ataka Kusalia United

Kiungo wa klabu ya Fiorentina ya nchini Italia anayekipiga ndani ya klabu ya Manchester United Sofyan Amrabat raia wa kimataifa wa Morocco amesema anatamani kuendelea kusalia United.

Amrabat ambaye yupo kwa mkopo klabuni hapo akitokea klabu ya Fiorentina ambapo mkopo wake umemalizika sasa baada ya mchezo wa fainali ya michuano ya Fa jana, Lakini alipoulizwa na wanahabari alionesha anahitaji kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Old Trafford.amrabat“Kwa mimi kubaki ndani ya Manchester United ni mpango wangu, tutaenda kuzungumza na klabu, Manchester United ni klabu kubwa duniani hivo hakuna ambaye hatataka kuendelea kucheza mahali hapa”

Mchezaji huyo amekua na kiwango bora sana kuelekea kumalizika kwa msimu jambo ambalo limewafanya mashabiki wa klabu hiyo kuamini kiungo huyo anastahili kupewa mkataba wa kuduma, Kwani mkataba wake una kifungu cha kumruhusu kununuliwa klabuni hapo na kiwango cha pesa kikiwa sio kikubwa.amrabatKama kiungo Sofyan Amrabat atafanikiwa kupewa mkataba wa kudumu ndani ya klabu hiyo itakua ni ndoto iliyokamilika, Kwani kiungo huyo amekua akisema mara kwa mara yeye kucheza ndani ya klabu hiyo ni kutimiza ndoto zake ambazo amekua nazo kwa muda mrefu.

Acha ujumbe