Amrabat: Niliitaka Man United Tu

Kiungo wa kimataifa wa Morocco anayekipiga kwa mkopo klabu ya Manchester United Sofyan Amrabat amesema vilabu kadhaa vilihitaji sana saini yake lakini kwake Man United ndio ilikua kipaumbele.

Amrabat ambaye ameanza katika kikosi cha Man United kwa mara ya kwanza jana katika ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Palace, Ameweka wazi kua akili yake ilikua inaiwaza Man United.amrabatKiungo huyo ambaye dili lake lilikamilika siku ya mwisho ya usajili na hiyo ilitokana na yeye kuweka msimamo mgumu kua anataka kucheza Man United tu, Kwani kuna vilabu kadhaa vilimfata na klabu yake ya Fiorentina lakini kiungo huyo aliieleza klabu yake kua anataka kucheza Man United tu.

Kiungo huyo ameonesha uwezo mkubwa jana katika mchezo wa kombe la Carabao licha ya kuchezeshwa kama beki wa kushoto, Huku akisisitiza kua kucheza Manchester United ni ndoto yake tangu akiwa mdogo na sasa ndoto imetimia.amrabatKiungo Sofyan Amrabat baada ya kucheza mchezo wake wa jana mashabiki wa klabu hiyo wameonesha kuvutiwa na kiwango chake kwa kiwango kikubwa, Huku wakiamini ushirikiano wake na kiungo Casemiro katikati utakua na msaada sana kwa klabu hiyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.