Kiungo mpya wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Morocco Sofyan Amrabat ameripotiwa kupata majeraha ambayo haijafahamika yatamueka nje ya uwanja kwa muda gani.
Kiungo Amrabat ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kutokana na majeraha ambayo bado hayajawekwa wazi na klabu yake ya Manchester United.
Hizi zinaendelea kua taarifa mbaya kwa klabu ya Man United kutokana na hali inayoendelea klabuni hapo, Kwani wachezaji kadhaa wa klabu hiyo wameshapata majeraha mpaka sasa na kiungo kuongezeka ni pigo jingine pia.
Kiungo huyo anaungana na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kama Mason Mount, Raphael Varane, Luke Shaw, Tyrell Malacia ambao wanauguza majeraha yao waliyoyapata siku za hivi karibuni.
Kiungo Sofyan Amrabat ambaye alisajiliwa siku ya mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa taarifa juu ya majeraha yake zilianza tangu alipojiunga na timu hiyo, Lakini ikaonekana kama taarifa za uzushi mpaka kiungo huyo alipoenguliwa kwenye timu ya taifa ya Morocco.

