Beki wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Ureno Nuno Mendes anatarajiwa kua nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne kutokana na majeraha ambayo ameyapata katika goti la kushoto.
Beki Nuno Mendes ambaye hajacheza mchezo hata mmoja tangu mwezi Aprili mwaka huu inaelezwa atakosekana uwanjani kwa miezi mingine minne kutokana na upasuaji ambao atafanyiwa kutokana na majeraha yake.Klabu ya PSG kupitia jopo la madaktari wa klabu hiyo wameamua kua beki huyo afanyiwa upasuaji nchini Finland, Hiyo ni kutokana na kuangalia maendeleo ya afya yake na wakaona anastahili kufanyiwa upasuaji ili aweze kukaa sawa.
Beki huyo wa kimataifa wa Ureno amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo, Lakini jinamizi la majeraha limekua sio rafiki kabisa kwake kwani amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yanamueka nje ya uwanja kwa muda mrefu.Beki Nuno Mendes sasa atakua nje ya uwanja kwa miezi minne hii inadhihirisha kua hatacheza mpira tena ndani ya mwaka huu mpaka mwaka 2024, Hivo klabu yake ya PSG na timu ya taifa ya Ureno wote watakosa huduma yake kwa kipindi hichi.