Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo kwajili ya kumpa mkataba kiungo kinda wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Tunisia Hannibal Mejbri ambaye mkataba wake wasasa unaisha mwaka 2024.
Manchester United inataka kiungo huyo aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu na ndio maana wanafanya mazungumzo na kambi ya kiungo huyo ili kuweza kumaliza suala hilo.Mkataba wa sasa wa kiungo huyo unamalizika mwaka 2024 na kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja hadi mwaka 2025, Lakini Man United wanahitaji kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi kiungo huyo.
Kiungo huyo raia wa kimataifa wa Tunisia ameonesha kiwango kizuri katika michezo kadhaa aliyocheza msimu huu, Huku akimvutia kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag na kuhitaji kiungo huyo aongezewe mkataba wa muda mrefu zaidi klabuni hapo.Kiungo Hannibal Mejbri ambaye alikua kwa mkopo klabu ya Birmingham msimu uliomalizika na kurudi kwenye timu msimu huu, inaelezwa alihitajika kutolewa kwa mara nyingine lakini kocha Ten Hag alitaka mchezaji huyo abakie Manchester United na kumuahidi muda wa kuceza zaidi.