Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameweka wazi klabu ya Real Madrid haitasajili kupata mbadala wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Toni Kroos ambaye anastaafu mwishoni mwa msimu huu.
Toni Kroos ambaye ameagwa kwenye mchezo wake wa mwisho jana katika dimba la Bernabeu ametangaza kustaafu soka mwishoni msimu huu, Huku kocha Ancelotti akiulizwa kama klabu hiyo itapata mbadala wake.Kocha huyo alichosema kua ni ngumu kupata mchezaji mwenye ubora wa Kroos, Hivo ni wazi klabu hiyo haitaingia sokoni kutafuta mbadala wa Kroos zaidi hata wakisajili kiungo basi watasajili kwasababu ya kuboresha kikosi chao.
Kocha huyo pia aliulizwa juu ya suala la Jude Bellingham kuweza kuvaa viatu vya Kroos, Lakini Ancelotti alisema kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza ni hatari zaidi kwenye eneo la mwisho zaidi kwa mara nyingine alionesha kua Kroos hatakua na mbadala wake.Toni Kroos ni wazi anaondoka klabuni hapo akiwa ameacha pengo kubwa kwani licha ya lundo la viungo waliopo klabuni hapo na ubora wao, Lakini bado hakuna kiungo ambaye anaonekana ana uwezo wa kuvaa viatu vya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani.