Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amefunguka juu ya kurejea kwa beki wake wa katikati Eder Militao raia wa kimataifa wa Brazil ambaye alikua anaandamwa na majeraha kwa muda mrefu.
Ancelotti amesema beki Militao yupo tayari kuanza kuitumikia klabu hiyo hivo anaweza kupata dakika katika michezo ijayo, Akiwakumbusha waandishi kua ameshawahi kumchezesha kiungo Sami Khedira kwenye mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa ulaya akiwa ametoka tu kwenye majeraha.Kocha huyo amesisitiza kua beki huyo yupo tayari na atapata nafasi katika michezo ijayo ya klabu hiyo, Lakini akaweka wazi kua Militao hayupo tayari kucheza dakika 90 lakini anaweza kucheza dakika kadhaa na akafanya vizuri.
Maswali yamekua mengi baada ya beki huyo kutopangwa katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mkondo wa kwanza dhidi ya Man City, Huku nafasi yake akicheza kiungo Aurelien Tchouameni.Baada ya kuwepo kelele nyingi juu ya Militao kutakiwa kuanza katika mchezo wa marudiano dhidi ya Man City wiki ijayo, Ndipo kocha Carlo Ancelotti alipojitokeza na kuwatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwaambia Militao yupo tayari na anaweza kupata nafasi katika michezo ijayo.