Klabu ya soka ya Southampton imefanikiwa kurejea kwenye ligi kuu ya Uingereza kwenye msimu wa 2024/25 baada ya kuitupa nje klabu ya Leeds United kwenye mchezo wa mtoano.
Southampton leo imefanikiwa kupata ushindi wa goli moja kwa bila katika mchezo uliopigwa katika dimba la Wembley ushindi ambao moja kwa moja umewapa tiketi ya kurejea kwenye ligi kuu ya Uingereza.Klabu hiyo ilimaliza msimamo wa li ya Championship wakiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo huku wapinzani wao klabu ya Leeds United wao wakiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Leicester City na Ipswich Town.
Mchezo wa leo ulikua wa mtoano ambapo ambaye alikua anashinda ndio alikua anapata nafasi ya kupanda kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa mara nyingine, Kwani vilabu hivi vilishuka kwa pamoja msimu wa mwaka 2022/2023.Goli pekee la mshambuliaji Adam Amstrong dakika ya 24 mapema tu katika mchezo huu lilitosha kuwarudisha watakatifu hao wenye maskani yao St. Marry Park kunako ligi kuu ya Uingereza. Hivo ni wazi timu zilizopanda ligi kuu msimu huu ni Leicester City, Ipswich Town, pamoja na Southampton.