Pavard Anaitaka Man United

Beki wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa Benjamin Pavard inaelezwa anataka kujiunga na klabu ya Manchester United ambayo nayo inaonesha kumuhitaji.

Beki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa inaelezwa hayuko kwenye mipango ya klabu ya Bayern Munich kuelekea msimu ujao, Huku akiwepo kwenye orodha ya mabeki ambao wanahitajika na klabu ya Man United.pAVARDManchester United wapo sokoni kuhakikisha wanapata beki wa katikati baada ya kukubali kumuachia beki wa kimataifa wa Uingereza klabuni hapo Harry Maguire, Hivo Benjamin Pavard anaingia kwenye orodha ya klabu hiyo kama moja ya warithi wa beki huyo.

Beki huyo inaelezwa ameonesha nia ya kujiunga na mashetani hao wekundu ndani, Lakini bado Man United hawajatuma ofa rasmi kwa klabu ya Bayern Munich ili kupata huduma ya beki huyo.pAVARDMan United pia wanawasiliana na kambi ya beki mwingine wa kimataifa wa Ufaransa Jean Clair Todibo ambaye anakipiga katika klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa hivo Pavard akikosekana badi Todibo atakua mrithi wa Harry Maguire.

Acha ujumbe