Kocha mkuu wa Real Betis Maunuel Pellegrini amesema kuwa ‘timu iliyocheza vyema zaidi ilishinda’ katika michuano ya Ligi ya Europa kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico Rome ambapo AS Roma walikuwa wenyeji wa mchezo huo.

AS Roma walitangulia kufunga bao baada ya kupata mkwaju wa penati kupitia Paul Dybala katika kipindi cha kwanza, lakini kabla hakijamalizika Real Betis walisawazisha bao hilo kupitia kwa Guido Rodriguez na kwenda mapumziko kwa sare ya moj kwa moja.
Baada ya kurejea kipindi cha pili Real Betis waliongeza kasi ya kupambana na kuondoka na alama tatu baada ya kufunga bao dakika ya 88. Pellegrini amesema kuwa;
“Tulikuwa bora kuliko Roma katika kipindi cha kwanza, ambapo kipindi cha pili kilikuwa cha usawa,” Pellegrini aliiambia Sky Sport Italia na katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Pellegrin amesema kuwa anadhani timu hiyo iliyocheza vizuri zaidi ilishinda, kwani wao pia walikuwa na nafasi nyingi za kufunga na kumiliki mpira mzuri dhidi ya mpinzani mwenye nguvu kwenye uwanja wao.
Betis wana assilimia kubwa ya kuongoza kundi lao la Ligi ya Europa wakiwa na pointi tisa, wakifuatiwa na Ludogorets pointi nne, Roma tatu na HJK Helsinki moja. Kulikuwa na ripoti katika maandalizi ya mechi kwamba huu ulikuwa mchuano mkali kati ya Pellegrini na Jose Mourinho, lakini makocha wote walipuuza mapendekezo haya.

Kocha huyo aliongeza kwa kusema kuwa yeye na Mourinho walikuwa na mechi nyingi pamoja Uhispania na Uingereza na hawakuwahi kuwa na shida za kibinafsi.

