Potter Juu ya Thiago Silva

Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter amesema kuwa anafurahia kufanya kazi na Thiago Silva ambaye ana uzoefu mkubwa lakini pia unyenyekevu wa kufanya kazi pamoja na kujituma uwanjani.

 

Potter Juu ya Thiago Silva

Siku si nyingi beki huyo wa kati alitoka kusema anafurahishwa na kocha huyo kwa jinsi ambavyo anawafundisha lakini pia amekuwa na maelewano mazuri na wachezaji wote ndani ya Chelsea.

Thiago ambaye ametimiza miaka 38 siku chache zilizopita amekuwa ni beki muhimu sana kwenye kikosi cha The Blues. Thiago alisajiliwa kipindi cha Frank Lampard akitoka klabu ya Psg na akafanikiwa kupata UEFA na mataji mengine ndani ya klabu hiyo.

Potter pamoja mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakimuhusudu sana Thiago kutokana na ubora wake anaouonyesha uwanjani licha ya umri wake mkubwa lakini ni panga pangua ya kikosi cha kwanza labad apate majeraha.

Potter Juu ya Thiago Silva

Potter baada ya kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi, Leo hii anamkaribisha Wolveshampton katika mechi yake ya pili pale Stamford Bridge huku msimu uliopita hakuna aliyekuwa mbabe kati yao.

Hali ya mkataba wa Thiago Silva ambaye ni Mbrazili  unatarajiwa kujadiliwa baada ya Kombe la Dunia ambalo linatarajiwa kupigwa November 2022.

Potter Juu ya Thiago Silva

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.