Rafael Varane Nje Mwezi Mmoja.

Ni kama Rafael Varane na Sergio Ramos wanakumbwa na madhila ya kuondoka Real Madrid. Majeraha yamekuwa yakiwaandama kwa sehemu kubwa msimu huu.

Kwa Ramos, kabla ya kusajiliwa PSG, alikuwa ni majeruhi. Mpaka sasa, beki huyo hajaitumikia timu hiyo kwenye mchezo wowote. Kumeanza kusambaa taarifa za klabu hiyo kuanza kufikiria uwezekano wa kusitisha mkataba wake na klabu hiyo.

Kule Old Trafford, Rafael Varane anarejea tena kwenye orodha ya majeruhi, muda mfupi baada ya kutoka kwenye orodha hiyo. Varane aliumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atalanta na sasa, United wameripoti beki huyo atakua nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja.

Varane anaumia wakati ambao United inamuhitaji zaidi kwenye safu yake ya ulinzi. The Red Devils watakutana na majirani zao, Man City wikiendi hii kabla ya kuwafata Watford na Villarreal baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe