Rasmi Vladimir Ivic Kocha mpya Watford.


Watford wamemteua Vladimir Ivic, 43, mikoba yao ya ukocha kwa mkataba wa mwaka mmoja. Kandarasi hiyo itarefushwa kutegemea matokeo yatakayosajiliwa na kikosi hicho cha Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) chini yake.

Ivic ambaye ni kocha wa zamani wa Maccabi Tel Aviv ya Israel anamrithi mkufunzi Nigel Pearson aliyetimuliwa na Watford zikiwa zimesalia mechi mbili pekee kwa kampeni za msimu huu wa 2019-20 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kukamilika rasmi.

 

Rasmi Vladimir Ivic Kocha mpya Watford.

Licha ya Pearson kupigwa kalamu wakati ambapo Watford walikuwa wakipigania nafasi finyu ya kusalia EPL, kikosi hicho kiliteremshwa ngazi baada ya kupoteza mechi zote mbili chini ya kocha mshikiliz Hayden Mullins.

Kichapo cha 3-2 walichopokezwa na Arsenal katika siku ya mwisho ya msimu kilitamatisha kipindi cha miaka mitano ya Watford waliotinga fainali ya Kombe la FA mnamo 2019 kunogesha kipute cha EPL.

Ivic hana tajriba yoyote katika soka ya Uingereza ama akiwa mchezaji au kocha japo Watford wamesisitiza kwamba wameridhishwa na mbinu zake za ukufunzi.

“Ni mara yangu ya kwanza nchini Uingereza na itanilazimu kuzoea mazingira haya mapya haraka iwezekanavyo kisha nijitahidi kurejesha Watford kwenye EPL,” akasema Ivic aliyewahi kuvalia jezi za timu ya taifa ya Serbia katika siku zake za uchezaji.

 

Rasmi Vladimir Ivic Kocha mpya Watford.

Ujio wake ugani Vicarage Road kunamfanya kocha wa nne wa Watford katika kipindi cha miezi 12 baada ya kutimuliwa kwa Javi Gracia na Quique Sanchez Flores mwanzoni mwa msimu huu. Kuondoka kwa wawili hao kulimpisha Pearson kuingia Watford mnamo Disemba 2019.

Ivic alisalia huru baada ya kuwaongoza Maccabi Tel Aviv kunyanyua mataji mawili ya Ligi Kuu ya Israel. Awali, alikuwa amedhibiti pia mikoba ya PAOK FC aliowanyanyulia ubingwa wa Greek Cup.

Ametua Watford pamoja na makocha watatu waliokuwa wasaidizi wake kambini mwa Maccabi Tel Aviv.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma Zaidi

27 Komentara

    Pambana uipandishe daraja.

    Jibu

    Vladmir ni safi ipaishe watford tunataka tuione epl tena

    Jibu

    Pongezi kwake Vladimir kutua Watford kawanyeshe Kaz mzee baba

    Jibu

    hongera Ivic nina imani utafanya vizuri watford

    Jibu

    Nigel Pearson kwa upande wangu namuona kocha mzur sana sema n mistake ambayo imetokea ila sio mbaya kwa upande wa Vladimir ivic kuwa kocha maana nae pia yuko vzur sana ninamatumain nae sana atasaidia Watford

    Jibu

    Vladimir Ivic ajipange kuirudisha Watford kwenye hadhi yake

    Jibu

    vladimir yupo vizuri sana katika ufundishaji soka

    Jibu

    Vladmir Ivic amepewa mkataba wa mwaka mmoja maana yake anatakiwa kuhakikisha kwamba Watford inarudi EPL vinginevyo hana chake#meridianbettz

    Jibu

    Yupo vizuri sana Vladimir katika ufundishaji soka#Meridianbettz

    Jibu

    saf

    Jibu

    Good

    Jibu

    Ni jambo zuri kwa wartfod mashabiki wanasubili mambo mazuri kutoka kwake.

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    All ze best coach

    Jibu

    Pongezi kwake

    Jibu

    Natumai utaitunza vyema na utaiweka watford katika nafasi nzuri

    Jibu

    Vladimir anakibarua kizito kuipandisha daraja Watford

    Jibu

    Ajipange vizuri ili timu isonge mbele#meridianbett

    Jibu

    Ni jambo zuri vladimir kutua watfod imekua kama bahati kwa watfod tunataka tuone kazi yako

    Jibu

    Ni kocha mwenye uwezo wake tunategemea mabadiliko kamkubwa sana kuiyona Watford kwenye ushindani

    Jibu

    Sawa sawa

    Jibu

    Ni kocha mzuri na anatakiwa kufanya vena zaidi mana kupewa mkataba Wa mwaka mmoja ni kama kupimwa uwezo wako ajitahidi sana uwe wa mafanikio zaidi

    Jibu

    Kila la heri

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Vladimir Ivic ajipange kuirudisha Watford kwenye hadhi yake

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.