Rice: Arteta Alikua Sababu ya mimi Kujiunga Arsenal

Mchezaji wa gharama zaidi kwenye klabu ya Arsenal Declan Rice amesema kocha wa klabu hiyo Mikel Arteta ndio alikua chachu kubwa ya yeye kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

Kiungo Declan Rice alijiunga na klabu ya Arsenal kwenye majira ya joto yaliyopita kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 105 ikiwa ni rekodi kubwa zaidi ya usajili tangu kuanzishwa kwa klabu ya Arsenal.riceKiungo huyo amesema wakati amekutana tu na kocha Arteta alitambua ndio kocha ambaye anaweza kufanya nae kazi katika kuendeleza mpira wake kutokana na namna kocha huyo alivyokua anazungumza na vilevile namna anavyouona mchezo wa soka.

Kiungo huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ambaye alikua nahodha wa klabu ya Westham United ilihitajika nguvu kubwa kumtoa kwa kwa wagonga nyundo wa London kutokana na ubora ambao alikua anauonesha klabuni hapo.riceDeclan Rice mpaka sasa amefanikiwa kuonesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Arsenal kwa michezo michache aliyocheza ndani ya timu hiyo msimu huu na hii inadhihirisha kua kocha Mikel Arteta ni kweli alikua mtu sahihi wa kuendeleza ubora wake.

Acha ujumbe