Kocha wa zamani wa vilabu vya Rb Leipzig na Bayern Munich Julian Nagelsmann anatajwa kama miongoni mwa makocha ambao wanaweza kurithi mikoba ya aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Ujermani Hans Flick.

Shrikisho la soka nchini Ujerumani jana lilitoa tamko la kumfuta kazi kocha Hans Flick kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya wa timu ya taifa ya Ujerumani na kocha Nagelsmann anaonekana kama mtu anaeweza kurithi mikoba hiyo.NagelsmannKocha Hans Flick ambaye alirithi mikoba ya kocha Joachim Low ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2021, Lakini mwenendo wa timu hiyo umefanya shirikisho la soka nchini humo kumfuta kazi kocha huyo.

Sababu kubwa iliyochochea Flick kufukuzwa kazi ni kipigo cha mwisho cha mabao manne dhidi ya timu ya taifa ya Japan, Huku ikikumbukwa pia timu ya taifa ya Ujerumani iliishia hatua ya makundi katika michuano ya kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar.NagelsmannKocha Julian Nagelsmann ambaye alifutwa kazi mwezi Machi ndani ya Bayern Munich anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kuifundisha timu ya taifa ya Ujerumani mpaka kwa maana hiyo inawezkana kocha huyo kijana akapewa jukumu la Hans Flick.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa