Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba amesema anataka kuwafanya wote wanaomponda wapate aibu kutokana na ambacho atakifanya uwanjani.
Kiungo Paul Pogba amekua akiandamwa na mashabiki wakiamini kua uwezo wake umeshuka na huenda umefika mwisho kabosa, Lakini kiungo huyo amepanga kuwafanya wote wanaomsema vibaya kwasasa wajutie maneno yao.Kiungo huyo tangu ajiunge na klabu ya Juventus msimu uliomalizika kumekua na maneno mengi na mengi yakimuandama kua uwezo wake umekwisha, Lakini yeye anaamini bado ana uwezo kuendelea kufanya vizuri na kuwafunga watu midomo.
Mfaransa huyo amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara tangu aliporejea Juventus ikiwa inaelezwa ni miongoni mwa sababu zinafanya mchezaji huyo ashindwe kuonesha makali kama ambayo alikua anaonesha miaka kadhaa nyuma.Paul Pogba ikumbukwe msimu taktibani wote uliomalizika aliutumia akiwa anauguza majeraha hivo hakupata nafasi ya kucheza muda mrefu, Hivo upande wake anaamini msimu huu ndio wakati wa kuwafunga midomo wote wanaomponda.