Veratti Rasmi Atua Qatar

Aliyekua kiungo wa klabu ya PSG Marco Veratti raia wa kimataifa wa amefanikiwa kujiunga na klabu ya Al Arabi ya nchini Qatar baada ya kumalzina na waliokua waajiri wake klabu ya PSG.

PSG inaelezwa haikua tayari kumuchia kiungo huyo katika dirisha hili aondoke klabuni hapo, Lakini kiungo huyo amefanikiwa kushinikiza na kuondoka ndani ya Viunga vya Parc de Prince.verattiKiungo Marco Veratti amekua moja ya wachezaji muhimu wa klabu ya PSG kwa kipindi kirefu na kupata mafanikio na klabu hiyo, Lakini ameona ni wakati sahihi wa kuondoka ndani ya timu hiyo na kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia anatarajia kufanya vipimo vya afya kesho na kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia klabu ya Al Arabi ya nchini Qatar kama mchezaji mpya ndani ya klabu hiyo.verattiKiungo Marco Veratti alikua akihitajika na vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia,Lakini klabu ya Al Arabi imeonekana kuibuka mshinda katika kinyang’anyiro cha kumpata kiungo huyo fundi kutoka klabu ya PSG.

Acha ujumbe