Marco Veratti Kutimkia Saudia

Kiungo wa kimataifa wa Italia anayekipiga klabu ya PSG ya nchini Ufaransa Marco Veratti anakaribia kutimkia katika klabu ya Al-Hilal ya nchini Saudia Arabia.

Marco Veratti mpaka sasa inataarifiwa ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Al-Hilal, Hivo kinachosubiriwa ni klabu hiyo kutoka nchini Saudia kupeleka ofa mezani kwa klabu ya PSG kwajili ya kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Italia.Marco verattiKiungo huyo fundi ambaye ameitumikia klabu ya PSG kwa muda mrefu anaona ni wakati wa yeye kwenda kutafuta changamoto mpya klabu nyingine na klabu hiyo ni Al-Hilal kutoka nchini Saudia Arabia.

Kiungo Marco Veratti inaelezwa amekubaliana na Al-Hilal mkataba wa miaka mitatu ambapo klabu ya PSG wao wanaelezwa hawapo tayari kupokea kiasi cha Euro milioni 30 ambayo klabu hiyo Saudia inataka kutuma.Marco verattiRais wa klabu ya PSG Nasser El Khelafi ndio anasubiriwa aruhusu uhamisho huo uweze kukamilika na klabu ya Al-Hilal wanatarajiwa kuongeza dau ambalo wameliweka mpaka wakati huu kwani Nasser hakua tayari kupokea kiasi kilichowekwa mwanzo.

Acha ujumbe