David Silva Atundika Daluga

Kiungo fundi raia wa kimataifa wa Hispania aliyewahi kukipiga katika vilabu vya Valencia, Manchester City, na Real Sociedad na timu ya taifa ya Hispania David Silva ametundika daluga rasmi.

David Silva rasmi ametangaza kuachana na soka rasmi leo akiwa katika klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania ambayo ameitumikia kwa misimu miwili baada ya kuondoka klabu ya Manchester City ambapo aliweka heshima kubwa.david silvaKiungo huyo wa kimataifa wa Hispania anayefahamika kwa jina la utani kama El Mago amecheza michezo takribani 869 akifunga mabao 156 na pasi za mabao 226 akifanikiwa kushinda mataji 20 kama mchezaji.

Mchezaji huyo fundi kabisa kuwahi kutokea katika soka la Hispania amecheza kwa mafanikio makubwa katika vilabu alivyovitumikia pamoja na timu ya taifa ya Hispania na kushinda mataji takribani yote makubwa ambayo amewahi kuyapigania.david silvaKiungo David Silva ametangaza kustaafu soka akiwa kwenye kikosi cha Real Sociedad lakini kiungo huyo atakumbukwa zaidi kwenye klabu ya Man City ambapo ndani ya klabu hiyo amefanikiwa hadi kutengenezewa sanamu ndani ya timu hiyo.

 

 

Acha ujumbe