Klabu ya soka ya PSG mabingwa wa soka nchini Ufaransa wana kibarua kizito kwa mshambuliaji wao nyota klabuni hapo Kylian Mbappe ambaye wamemueka kando.
Jana PSG walitangaza kumueka pembene Mbappe kwenye ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya ambayo wataifanya nchini Japani na lengo likiwa ni kuhakikisha wanamuuza mchezaji huyo katika dirisha hili la usajili.Mabingwa hao wa Ufaransa wanatamani kwa kiwango kikubwa vilabu vingine barani ulaya watume ofa ya kumtaka mchezaji huyo, Lakini changamoto ni kua wanatambua klabu pekee ambayo mchezaji huyo anataka kucheza ni Real Madrid.
PSG wanakua kwenye wakati mgumu kwakua wamegundua nia ya Mbappe ni kuondoka klabuni hapo bure mwishoni mwa msimu ujao, Huku kitendo hicho klabu hiyo haikubaliani nacho na kumueka sokoni mchezaji huyo.Klabu ya PSG imemueka kando Mbappe kuonesha hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu lakini changamoto itakuja pale ambapo klabu ya Real Madrid itashindwa kufikia dau ambalo mabingwa hao wa Ufaransa wamelieka kwani timu zingine haziwezi kuweka dau kwakua zinaelewa kua Mbappe anataka kucheza Real Madrid.