Klabu ya Manchester United jana ilifanikiwa kuifunga klabu ya Arsenal katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu uliopigwa nchini Marekani.
Mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo katika dimba la Metlife nchini Marekani Manchester United walifanikiwa kushinda kwa mbao mawili kwa bila ambapo magoli yalifungwa kipindi cha kwanza na nahodha Bruno Fernandes na Jadon Sancho.Man United ambayo haikua inamiliki sana mpira katika mchezo huo lakini walionekana kutumia nafasi zao vizuri katika kipindi cha kwanza na kuimaliza mechi ambayo ilimalizika kwa wao kushinda mabao mawili kwa bila.
Arsenal kwa upande wao walionesha mchezo mzuri lakini umahiri wa safu ya ulinzi ya Manchester United uliwanyima nafasi ya kupata magoli, Lakini licha ya Man United kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila mwishoni kwa mchezo huo palipigwa mikwaju ya penati.Klabu ya Manchester United ilifanikiwa kushinda mara mbili jana baada ya kushinda kwa mabao mawili kwa bila ndani ya dakika 90 za mchezo, Lakini pia walifanikiwa kushinda katika mikwaju ya penati ilyopigwa baada ya mchezo ambapo ilikua mikwaju 5-3.