Arsenal Dhidi ya Manchester United Usiku wa Leo

Klabu ya Arsenal leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Manchester United katika mchezo wa kirafiki ambao pia ni maalumu kwa maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa 2023/24.

Arsenal baada ya kucheza michezo yake miwili na kufanikiwa kupata ushindi mchezo mmoja na kusuluhu mchezo mmoja wanaenda kumenyana na Man United ambao mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo yao yote miwili ya kirafiki.RiceMtanange huo ambao utapigwa nchini Marekani ambapo timu hizo zipo kwajili ya maandalizi yao kuelekea msimu ujao, Mchezo huu umevuta hisia za mashabiki sana haswa ukizingatia ni moja ya vilabu hasimu zaidi kutoka nchini Uingereza na vina mashabiki wengi.

Kuelekea mtanange huu kati ya Arsenal na Man United kocha wa klabu ya United Erik Ten Hag jana akiongea na wanahabari alisema kwao mchezo huu hawatauchukulia kama wa kirafiki bali watakwenda kucheza kama mchezo muhimu kwao.RiceMchezo huu unatarajiwa kua na mvuto na mgumo licha ya kua wa kirafiki kwani kauli ya kocha Ten Hag imeshaonesha kua wameutafsiri mchezo huu kwa namna gani na kwa upande wa Arsenal nao hawatauchukulia mchezo huu kiuwepesi kutokana na uhasimu uliopo baina ya vilabu hivi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.