Aliyekua mchezaji wa klabu ya Al-Ahly ya nchini Misri Luis Jose Miquisonne ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Simba mapema leo.
Luis Jose Miquisonne baada ya tetesi za muda mrefu kua anarudi kuitumikia klabu ya Simba hatimae yametimia kwani leo saa saba mchana klabu ya Simba kupitia mitandao yake ya kijamii walitangaza urejeo wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo raia wa kimataifa wa Msumbiji alifanikiwa kuitumikia klabu ya Simba kwa misimu miwili na nusu kabla ya kutimkia klabu Al-Ahly na kukaa nje ya klabu hiyo kwa miaka miwili na sasa kurejea rasmi ndani ya klabu hiyo.
Miquisonne alifanikiwa kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Al-Ahly wiki iliyomalizika na kufanikiwa kurejea ndani ya klabu ya Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili na kua mchezaji ghali zaidi kikosini.
Mshambuliaji Miquisonne baada ya kutambulishwa leo kurejea ndani ya klabu ya Simba taarifa zinasema wiki ijayo atakua tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uturuki kuungana na wachezaji wenzake ambapo maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao yanaendelea.

