Miquisonne: Nikirudi Tanzania Ni Simba Tu

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba anayekipiga katika ya Al Ahly kwasasa Luis Josee Miquisonne amesema kama atapata nafasi ya kurejea Tanzania basi klabu pekee atakayocheza ni Simba tu.

Mchezaji huyo ambaye amewahi kukipiga ndani ya klabu ya Simba kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu ya Simba kabla ya kutimkia ndani ya klabu ya Al Ahly ya nchini Misri, Ameweka wazi kua kama itafika wakati anataka kurejea Tanzania basi klabu pekee atakayocheza ni Simba wekundu wa msimbazi.miquisonneKumekua na taarifa ambazo zimekua zikiendelea siku za hivi karibuni kua mchezaji Luis Josee Miquisonne amemalizana na klabu ya soka ya Yanga, Lakini yeye mwenyewe ameweka wazi kua hawezi kucheza klabu tofauti na Simba kama ikitokea anarudi Tanzania.

Winga huyo hatari amekua akifukuziwa na klabu ya Simba kwa muda mrefu wakitaka kumrejesha nyumbani, Na hii inatokana na winga huyo wa kimataifa wa Msumbiji kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa miamba ya soka barani Afrika klabu ya Al Ahly.miquisonneLuis Josee Miquisonne ni kama amepita kwenye njia za mchezaji mwenzake aliecheza nae Simba Clatous Chama, Kwani Chama kabla ya kurejea nchini akitokea Rs Berkane alitoa kauli ya namna hii kua kama akirejea Tanzania basi klabu pekee atakayocheza ni Simba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.