Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Argentina Lisandro Martinez amerejea ndani ya klabu ya Manchester United baada ya kumaliza kushangilia ubingwa na timu ya taifa ya Argentina.
Beki huyo amekua mchezaji wa mwisho kuripoti kwenye kambi ya klabu hiyo kati ya wachezaji wote waliokua wameshiriki michuano ya kombe la dunia, Lakini hiyo ni kwasababu timu yake imefanikiwa kushinda ubingwa hivo walikua walikuaa muda wa kushangilia ubingwa huo.
Beki Lisandro Martinez ambaye alikua miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina chini ya kocha Lionel Scaloni ambacho kimefanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia, Na rasmi mchezaji huyo amerejea kwenye kambi ya United kuungana na wachezaji wenzake.
Mchezaji huyo ambaye leo amerejea kwenye kambi ya Man United anatarajiwa kuwepo kwenye mchezo wa jumamosi wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Wolverhampton, Kwani beki huyo amekua moja wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Man United.
Kurejea kwa Lisandro Martinez ndani ya Manchester United ni faraja kubwa kocha wa timu hiyo Erik Ten Hag, Kwani kocha huyo alilazimika kumpanga Luke Shaw kama beki wa kati katika mchezo wa jana dhidi ya Nottingham Forest kutokana na kukosa chaguo sahihi la beki wa katikati.

