Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amesema kua klabu hiyo bado inahitaji huduma ya mchezaji wao raia wa kimataifa wa Ureno Joao Felix.
Kiungo Joao Felix amekua kwenye kiwango bora sana msimu huu ndani ya klabu hiyo japo klabu hiyo haipo kwenye nafasi nzuri, Lakini ubora huo pia alifanikiwa kuuhamishia timu ya taifa ya Ureno kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.
Joao Felix amekua akihusishwa kuondoka ndani ya Atletico madrid mara kwa mara huku vilabu kadhaa vikihusishwa, klabu ya Manchester United inatajwa kua karibu zaidi kwenye kuhakikisha inanasa saini ya mchezaji huyo.
Kocha wa klabu hiyo Diego Simeone amemzungumzia mchezaji huyo wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi kuu nchini humo La liga dhidi ya klabu ya Elche, Na amesema ana mahusiano mazuri ya kikazi na mchezaji huyo na kusisitiza ni mchezaji muhimu kwenye timu.
Kocha Simeone aliendelea kwa kusema kua kama Joao Felix atahamisha kiwango ambacho amekionesha kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Atakua mchezaji muhimu zaidi na kusema mchezaji huyo ana kipaji kikubwa na timu inahitaji ubora wake.

