Olympique Lyon Wamtimua Blanc

Klabu ya Olympique Lyon imetangaza kumfuta kazi aliyekua kocha wake Laurent Blanc baada ya klabu hiyo kutokua na matokeo mazuri katika michezo yake ya ligi kuu ya Ufaransa.

Olympique Lyon wamekua hawana matokeo ya kuridhisha tangu kuanza kwa ligi kuu ya Ufaransa, Hivo klabu hiyo ikaamua kumuondoa kwenye kazi kocha wao huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa.olympique lyonLaurant Blanc aliiongoza klabu hiyo vizuri msimu uliomalizika lakini msimu huu hali inaonekana kubadilika na hali ilikua mbaya zaidi walipopoteza mchezo wakiwa katika dimba lao la nyumbani dhidi ya klabu ya PSG jambo lililowakasirisha mashabiki wa klabu hiyo.

Mashabiki wa klabu hiyo walikasirishwa na kitendo cha kupoteza mchezo katika uwanja wao wa nyumbani tena kwa kipigo cha aibu kutoka kwa PSG tena ikiwa mchezo wao wa nne kucheza bila kupata matokeo ya ushindi msimu huu.olympique lyonKlabu ya Olympique Lyon baada ya kumfukuza kocha Blanc ambaye amewahi kuifundisha klabu ya PSG kwenye taarifa yao wameelza kua klabu hiyo itamtangaza mbadala wa kocha huyo mapema iwezekavyo.

Makala iliyopita

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.