Lyon: Kwaheri Dembele, Karibu Slimani.

Klabu ya Lyon inayocheza ligi soka nchini Ufaransa – Ligue 1, imethibitisha kuondoka kwa Moussa Dembele na kumkaribisha Islam Slimani .

Dembele amejiunga na Atletico Madrid kwa mkopo huku akitazamia kusajiliwa kwa mkataba wa mojamoja mwishoni mwa msimu. Slimani anatua Lyon akitokea Leicester City kama mchezaji huru.

Moussa Dembele.

Atletico walihamishia nguvu zao kwa Dembele baada ya Napoli kukataa ofa ya timu hiyo kwa mshambuliaji Arkadiusz Milik ambaye alitazamiwa kama mbadala wa Diego Costa.

Usajili wa timu hizi ni kama mfumo wa daladala, abiria mmoja akishuka-mwingine anapanda. Waswahili husema “kinatoka kitu,kinaingia kitu”

Islam Slimani (katikati)Diego Costa alikatisha mkataba wake na Atletico Madrid, Simeone akaona isiwetabu – kamsajili Dembele, kule Ufaransa nao wakaona sio tatizo- wakamvuta Slimani.

Dembele anakwenda kuungana na Luis Suarez pamoja na Jao Felix katika safu ya ushambuliaji kule Wanda Metropilitano wakati ambapo Slimani ataungana na Depay katika kuhakikisha Lyon wanaendelea kuwachachafya PSG kwenye mbio za ubingwa msimu huu.


MERIDIANBET INAKUPA NAFASI YA KUWA MILIONEA KWA KILA BAADA YA DAKIKA 5

Mchezo wa Keno unakupatia fursa ya kuibuka kidedea kupitia droo zinazochezwa kila baada ya dakika 5 tu!! Tunaposema Meridianbet ni nyumba ya mabingwa, tunamaanisha!!

INGIA MCHEZONI

18 Komentara

    Duh dembele alikuwa poa sana

    Jibu

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    Slimani kiwango kimeshuka sana

    Jibu

    Ndembele alikuwa vizur

    Jibu

    Asant san kwa taarifa

    Jibu

    nc

    Jibu

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    Pole Sana Dembele

    Jibu

    Sliman atakiwasha

    Jibu

    Usajili wa timu hizi ni kama mfumo wa daladala, abiria mmoja akishuka-mwingine anapanda. Waswahili husema β€œkinatoka kitu,kinaingia kitu

    Jibu

    sliman atakiwasha

    Jibu

    Bonge ladili kwadembele

    Jibu

    Kambi popote

    Jibu

    Dembele asingetolewa kwenye kikosi

    Jibu

    Sliman kazi kwake sasa kuziba pengo

    Jibu

    Maisha popote

    Jibu

    Dembele atabaki kuwa bora

    Jibu

    Slimani nae yupo juu

    Jibu

Acha ujumbe