Winga na nahodha wa zamani wa klabu ya Manchester United Antonio Valencia amemsifia kinda wa klabu hiyo Alejandro Garnacho kutokana na ubora ambao anaouonesha klabuni hapo.
Valencia anasema anamuona Garnacho anaimarika siku baada ya siku huku akimuona akiweza kufanya makubwa zaidi siku za usoni, Hii inanaonesha ni namna gani watu wameeka matumaini kwa kinda Garnacho.
Kinda Garnacho ambaye alipata muda wa kucheza zaidi kwenye kikosi cha Manchester United msimu uliomalizika, Hii imefanya watu wengi kuamini mchezaji huyo atakuja kufanya makubwa katika kikosi cha Man United kama ataendelea kuonesha ubora.
Mkongwe Valencia anaamini mashabiki wa Manchester United wanatamani kumuona Garnacho anacheza kwasababu ya uwezo ambao amekua akiuonesha na wanaamini anastahili kupata nafasi hiyo.
Winga Alejandro Garnacho amekua akiaminiwa na kocha Erik Ten Hag licha ya umri wake mdogo, Hii inakumbusha mashabiki wa Man United kipindi cha gwiji Cristiano Ronaldo alipoaminiwa kwenye umri mdogo na Sir Alex Ferguson na akafanikiwa kufanya makubwa klabuni hapo.

