Kocha wa klabu ya Valencia Gennaro Gattuso anaamini kuwa klabu yake itafanikisha kumsajiri mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Edinson Cavani kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.

Edinson Cavani ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Manchester United msimu uliyopita, amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa nchini Hispania huku Valencia na Real Sociedad wakionesha kuvutiwa zaidi na mchezaji huyo.

Valencia, Valencia Kumsajiri Edinson Cavani, Meridianbet

Gatusso akizungumza kwenye mchezo leo Jumatatu alisema: “Mimi ni mtu wa matumaini kiuhalisia, tunafanya kazi, nikizungumza, nadhani tuna nafasi.

Peter Lim anafanya kazi sana na nadhani tunaelekea kumsajiri Cavani kwa sababu Lim anaimani kwenye nafasi zote.

“Unapomzungumzia Cavani, sio mchezaji wa kawaida, amechezea klabu kubwa na zenye viwango vya juu kwa muda mrefu. Ana miaka 35, lakini bado yuko vizuri kiutimamu, nazimgumzia maswala ya kiufundi, sio pesa, hilo sio tatizo langu na ni vitu viwili tofauti.

“Tatizo ni kwamba watu wengi wanazungumza pindi ukiwa kwenye mchakato na haiwezi kukamilika ndani ya dakika mbili.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa