Nagelsmann: Itakua Ngumu Kumzuia Haaland Kuliko Mbappe

Kocha wa klabu ya Bayern Munich Julian Nagelsman amesema kua kumzuia mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland katika mchezo wao wa robo fainali itakua ngumu kuliko ilivyokua kwa Mbappe wa PSG.

Klabu ya Fc Bayern Munich itakabiliana na Manchester City katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya katika hatua ya robo fainali, Ambapo kocha Nagelsmann anatarajia mchezo mgumu kutoka kwa wapinzani wao huku akimuona Haaland kama mchezaji hatari zaidi kuelekea mchezo huo.nagelsmannKlabu ya Bayern Munich itaanzia ugenini katika dimba la Etihad mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali na kumalizia nyumbani katika dimba lao la nyumbani la Allianz Arena, Hivo inaweza kua faida kwa mabingwa hao wa Ujerumani ambao wamekua na historia nzuri na michuano hiyo.

Kocha Nagelsman mbali na kuona Haaland ni mchezaji mgumu kukabiliana naye kuliko Mbappe wa klabu ya PSG, Lakini akisema kua amefurahia droo hiyo dhidi ya klabu ya Manchester City kwani ili uweze kubeba taji hilo wanatakiwa kuzifunga timu kubwa na wao wamejiandaa kwa hilo.nagelsmannNagelsman pia amesema anavutiwa na kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola raia wa kimataifa wa Hispania akimfutilia kwa timu zote ambazo amefundisha tangu akiwa Barcelona, Lakini akiweka kua hajawahi kumuiga kocha huyo kwenye mbinu zake za ufundishaji.

Acha ujumbe